“UPENDO WA MUNGU BABA TIBA YA KUJICHUKIA NA KUWA HURU DHIDI YA MAUMBO YA MIILI YETU.”
Shalom Wana wenye Roho wa Mungu! Roho wa Uzima na Amani. Hakika, nimejua kuwa tiba pekee ambayo watu wa kila rangi, rika, kabila, familia, na taifa dhidi ya changamoto yoyote ile ni KUUJUA na KUFUNULIWA UPENDO WA MUNGU BABA katika maisha yao.
Hapo awali nilijichukia mno, nilichukia umbo la mwili wangu, hii haikuja tu bali kwasababu niliwasikia watu walionizunguka na wanafunzi wenzangu. Ninakumbuka nikiwa shule nikioga kumbe kulikuwa na mwenzangu akinichungulia, na baadae nikasikia sauti ikiinuka na kusema “mmmh! Una umbo baya kweli”.
Ukweli nilijisikia vibaya mno, kauli hii iliniumiza na kunitesa sana, ilinifanya nijichukie na nianze kuishi, kuvaa na kutembea kama mwanamme wakati mimi ni msichana. Nikaanza kuvaa nguo pana kuzidi mwili wangu, kukunja sura, kutembea kwa miondoko huku nikiondoka miondoko ya kiume hii yote kuficha kifua changu na umbo langu.
Niliishi katika mateso haya ya kujikinai, ya kujilinganisha mpaka hapo kupitia Roho Mtakatifu aliponifunulia upendo wa Mungu BABA kwa kuniambia “NINAKUPENDA HIVYO ULIVYO” Roho Mtakatifu alimtumia mwana na mrithi mwenza mwenzangu wa Mungu Baba katika Kristo Yesu kuniambia hivyo. Hakika, ninamtukuza Bwana kwa kuniweka huru, toka kuwa Tom boy hadi kuwa mlimbwende wa haja. Upendo wa MUNGU BABA NI UHURU.