Ushuhuda na Shuhuda za Bwana ni Urithi wetu, Vizazi Vyetu na Kwa Taifa Lake. [Zab 119:111]

Shalom Wana na ukuhani wa Kifalme wa Mungu Baba katika Kristo Yesu! Kipindi cha  SHUHUDA ni kipindi cha maajabu ya Roho  Mungu juu yetu Wana. Ni MAAJABU! Ninayo furaha ya kumshukuru Mungu Baba katika Kristo Yesu mbele yenu Wana na Urithi wake.

Hakika ni raha tupu darasani na Roho Mtakatifu wa Baba katika Kristo, ninakumbuka siku ya Jumapili nilikuwa nimechelewa kidogo, nilipofika nilikuta ibada imeshaanza na nilikuta maagizo kuwa tuseme neno ASANTE BABA, mimi niliketi mahali pa Urithi wangu, nyumbani pa Baba yangu, ila kichwani mwangu kulikuwa na mambo yangu nayawaza na kuyawazua, nilianza kusema ASANTE BABA kwa mdomoni tu, pia cha zaidi nilianza kumuorodheshea Baba mambo yale aliyonitendea na kumwambia ASANTE BABA. mara nikamuona Baba amesimama mbele yangu huku akiniambia toka hapo kitini njoo ulale hapa Chini. Nilinyanyuka na kulala kifudifudi hapo chini. Nikiwa hapo, nikataka kunena kwa lugha lakini Baba akaniambia nyamaza kimya! Nikataka kuendelea kusema ASANTE BABA, akaendelea kunisisitiza kuwa ninyamaze KIMYA anataka kunielekeza jambo, niwe nafanya kama Yeye Baba yetu wa mbinguni anavyotka nifanye). Mwana hufanya yale amuonayo Baba akifanya au sema. (Yoh 4:34, 5:17-26).

Nikatii, nikawa namsikiliza akaniambia  nifungue macho nimuone na niende kumkumbatia na kweli nikatii kama vile Baba alivyonimbia na nilivyofumbua macho mbele nilimuona Apostle Julius amemkumbatia  Our beloved spiritual father (Apostle Wilbert Maridadi ) nami nikaenda kumkumbatia Baba. Aisee!nilihisi kuna kitu cha utofauti sana na ndipo BABA akawa anambia niwaambie wana wake waje wamuone kwa sababu amekuja ,akawa anasema Baba amekuja nyumbani na niwaambie waje wamuone Baba .

Me : “Come and see our Daddy, our Daddy is here!” ( Mara nilipomuona Baba ikabidi na mimi niwaite wenzengu waje wamuone Baba). (Yoh 1:46). Uzooefu ni kama vile baba zetu wa kimwili wanavyo rudi nyumbani wakiwa wametoka kazini au safarini watoto  wanvowakmbilia kwa furaha, upendo na shangwe kwa sababu wanajua tu baba hawezi kuja hivi hivi mikono mitupu lazima amekuja na zawadi au chochote kitu, hivyo watoto huwakimbilia kuwapokea na kupokea zawadi toka kwa Baba. Kitendo hiki au hali hii mara nyingi sana nawaonaga kwa watoto wa kaka zangu wakisikia tu baba yao amekuja watakimbia hata kama walikua wanakula au wanacheza wataacha na watamfuata;  lakini kwa sisi kanisani Baba alivyokuja ilikua tofauti wana wa Mungu walikuwa wanamshangaa hadi Baba akawa ananambia hawajui thamani yangu na hawatambui umuhimu wangu ndio maana wananishangaa ,na kweli na mimi nikawa naangalia naona watu wanamshangaa hata vile nilivyo kuwa nawaambia fumbueni macho mumuone Baba bado watu wakawa wanashangaa tu.

Baba akasema na leo ametuletea zawadi na anataka atupatie zawadi alizotuletea, atuhudumieYEYE (MUNGU BABA) mwenyewe.

Baba akanambia niwaambie wana na ukuhani wake wa kifalme wasimame ,wamfurahie kwa kusema ASANTE BABA!, wamshangalie kwa sababu ilikuwa ni siku yake kwetu sio siku ya kuorodhesha mahitaji yetu kwake kwani YEYE  (Mungu) ni Baba na anatambua tayari na hakuna jambo lolote litakalotutenganisha kwake kwani Yeye (Mungu) ni Baba ambaye ni Shujaa na anatupenda (unconditional love). (Rumi 8:32-39). Akazidi kuniambia kuwa niwaambie na kuwatamkia neno 

SHALOM kwa sababu Baba anavyokuja nyumbani basi SHALOM ipo . Na akamalizia kwa kuniambia kuwa Lugha ya Mwana iliyo kuu kuliko lugha zote ni lugha ya shukrani kwa Baba yake.

Hallelujah! ninamshukuru Mungu Baba kwa kujifunua kwangu BABA WA SHALOM. neno ASANTE BABA ni ufunguo wetu wana wa Mungu Baba wa kumuona Baba katika KUSANYIKO la Wana la uzao wa mzaliwa wa kwanza Yesu Kristo. (Ebrania 12:22).  Neno Asante Baba halina sababu kwetu Wana na Urithi wake Mungu Baba. Ni alama yetu ya jivuno letu Wana uweponi mwa Baba yetu wa mbinguni. Ni alama ya uthamani wetu na uthamani wa Baba yetu wa mbinguni kuliko thamani zote. Mwana wa Mungu Baba, nikushauri miezi hii sita iliyobakia kuhitimisha mwaka 2022 weka kando kila mzigo mzito wa orodha ya Mambo mazuri aliyokutendea Baba katika Kristo Yesu na anza kwa kumwambia ASANTE SANA BABA!

Na:

Mchungaji wa Huduma Ya Kimataifa Ya Pete Ya Muhuri,  (Hagai 2:23).

Dar es Salaam, Tanzania, Makao makao.

Pst. Assenga Baby

Ukumbi: Majestic Hall, Sinza-Remy!