“Kutokumsikia Mungu Baba kwa mwana wa Mungu ni UYATIMA.”
Ninapenda kumshukuru Mungu Baba katika Kristo Yesu katikati ya sherehe ya kumsheherekea Mungu BABA na Upendo wake, mwezi OKTOBA kila mwaka. Masikio yangu ya ndani, na nje yalizibuliwa na kuweza kumsikia akizungumza nami. Alizungumza nami kuhusu maisha yangu ya utotoni niliyoyapitia kwa kunionesha maono ya makala fupi ya safari yangu tangu utotoni, changamoto nilizokuwa nimezipitia, matendo mabaya niliyopata toka kwa watu wa karibu yangu na walezi wangu.
Hata nilipokuwa mkubwa nilijua kuwa nimepona, Roho Mtakatifu baada ya kunionesha akaniambia kuwa nimekukumbusha na kukuonesha hivi siyo kukumiza bali kukuponya, na ujue kuwa MIMI (MUNGU) NI BABA YAKO WA MILELE, NA NILIKUWA PAMOJA NAWE katika safari yako ya maisha yote, akazidi kuniambia kuwa SASA, NIMELIFUNUA PENDO LANGU KWAKO KAMA BABA YAKO ili upone, historia iwe mpya na uachane na historia hiyo ya zamani na UANZE KUFURAHIA UTAJIRI NA UFALME WANGU katika UPENDO WA BABA YAKO MIMI MUNGU”.
Hakika, baada ya makala hiyo ya kuona na kumsikia Mungu BABA nilisikia kuponywa moyoni mwangu, na kuwa na amani, na kusamehe kwa upesi sana.
Hakika, BWANA NA MFALME WETU ELOHIM ni JEHOVA RAPH, Upendo wake ni AFYA, ni DAWA, inaponya mifupa na viungo kwavyo hakuna dawa au maneno tupu ya mwanadamu yaweza kuponya. Ninamtukuza BWANA NA BABA YANGU WA MBINGUNI KATIKA KRISTO YESU kwa SAUTI YAKE, hakika sauti ya BABA ni tiba kwa mwana. Ninamtukuza Mungu BABA kwa kuwa katika Taifa lake ambalo linahimiza Wana na Ukuhani wake wa Kifalme kumsikia na kumsikiliza binafsi kabla au badala ya kumtegemea mchungaji au nabii, mwinjilisti au mwalimu, mtume peke tu.
Hakika, sauti ya MUNGU BABA KATIKA KRISTO YESU NI AMANI TIBA YA roho ya uyatima na mahangaiko yote.
Mwana wa Mungu. Taifa la Bwana, Ptm
Dar es salaam, Tanzania.
Soma zaidi.
Yoh 10:1-5.
One thought on “Ushuhuda na shuhuda za Bwana wetu Yesu Kristo ni Urithi wetu na uzao wetu. Zab 119:111”
Sauti ya Mungu Baba ni kalamu ya historia mpya ya ukuu juu ya nchi. Historia isiyo na uyatima bali Upendo utawalao juu ya mambo yote.
Asante sana kwa Ushuhuda huu kwa hakika Upendo wa Mungu Baba ni tiba dhidi ya moyo wa uyatima na kukosa makao. Ninapendwa na Mungu Baba kwa Upendo wa milele!
Sauti ya Mungu Baba ni kalamu ya historia mpya ya ukuu juu ya nchi. Historia isiyo na uyatima bali Upendo utawalao juu ya mambo yote.
Hakika!
Sauti ya Upendo wa Baba kwetu Wana ni Uponyaji!
Kwa sababu ya Upendo wake siku zote tuna furaha!
Sauti ya Mungu Baba kwa mwana ni pumziko tena ni Raha.
Asante kwa Ushuhuda huu umenijenga na kuniinua.
Wana tumetulizwa kifuani mwa Upendo wa Mungu Baba. Hapa ni mahali petu pa raha na shangwe!
Asante sana kwa Ushuhuda huu kwa hakika Upendo wa Mungu Baba ni tiba dhidi ya moyo wa uyatima na kukosa makao. Ninapendwa na Mungu Baba kwa Upendo wa milele!